Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Hussein Al-Hajj Hassan, Mkuu wa Muungano wa Wawakilishi wa Baalbek-Hermel, wakati wa hafla iliyoandaliwa na sehemu ya “Halbata” katika eneo la tano, kwa ajili ya kuadhimisha “Siku ya Shahidi wa Mji wa Halbata” na kuwaenzi Masayyid wawili watukufu, mbele ya familia za mashahidi na kundi la wakazi wa mji huo, katika mji wa Baalbek kaskazini, kwenye Husainiya ya mji huo, alisisitiza kwamba; mradi unaoongozwa na Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Magharibi, Kiarabu na Kiislamu, kwa lengo la kukomesha Muqawama na Hizbullah, hadi sasa haujafikia malengo yake.
Hajj Hassan alisema: Sababu ya kushindwa mradi huu ni kuendelea hadi sasa mazungumzo kuhusu kuwekewa mipaka silaha na kunyang’anywa silaha; ikiwa wao, kama wanavyodai, walikuwa wamekwishaumaliza kabisa uwepo wa Hizbullah, kwa nini bado kuna kampeni kubwa kiasi hiki, mashinikizo, upotoshaji wa ukubwa wa mambo na vita? Hili linaonesha kwamba Muqawama, licha ya kukabiliana na vita vitatu vikubwa, haujamalizika.
Aliongeza: Sisi ni sehemu ya mhimili wa Muqawama katika eneo hili, na tunajivunia kuwa ndani ya mhimili huu ambao lengo lake ni kuwa na mamlaka juu ya eneo hili, Palestina na masuala ya wanyonge. Nchini Lebanon wapo baadhi ya watu ambao hawapendezwi na kauli hizi, kwa sababu wao ni sehemu ya mhimili wa Marekani; yaani mhimili wa shari na mshirika wa Israel, ambae analitumia vibaya eneo hili kwa manufaa yake.
Hajj Hassan pia alizungumzia hali ya ndani, na alipouliza kuhusu hatima ya “makubaliano ya mfumo wa msingi”, alisema: Marekani “imejiondoa” katika suala hili na imelihusisha na muda wa kufanyika uchaguzi wa Israel.
Alikosoa kupitishwa bajeti na Serikali, bila kuwepo ahadi yoyote ya kweli katika suala la makazi, ujenzi upya na urekebishaji wa miundombinu, licha ya Serikali kuzungumza mara kwa mara kuhusu miradi ya kusini na kurejea waliokimbia makazi yao.
Mwisho, alisema: “Mawaziri wetu ndani ya Serikali walipinga bajeti iliyopitishwa, kwa sababu haikuwa na mgao wowote wa kweli kwa ajili ya ujenzi upya, ukarabati au makazi. Sisi pia katika Bunge la Wawakilishi tutaendelea kuonesha upinzani wetu dhidi ya kutotengwa fedha zinazohusiana na masuala haya; kwa sababu Serikali ina wajibu gani kwa Walebanoni?”
Maoni yako